Mofimu
Karibuni katika kipindi cha leo ili tujifunze aina, mifano na matumizi ya mofimu katika lugha ya Kiswahili.
Mofimu ni nini?
Mofimu ni kipashio kidogo katika lugha ambacho hakiwezi kugawika zaidi bila kupoteza maana yake ya kisarufi.
Tofauti ya Kiambishi na Mofimu
Ikumbukwe kuwa kiambishi ni mofimu ambayo huongezwa kabla au baada ya mzizi wa neno ili kuwakilisha dhana fulani.Pia,kiambishi hujitokeza kama mofimu tegemezi. Tofauti kuu hapa ni kuwa mofimu huweza kujisimamia kiimaan(mofimu huru) ilhali kiambishi hutegemea viambishi vingine ili kukamilisha maana.
Sifa za Mofimu
Kutokana na maelezo haya tunaweza kuorodhesha sifa zifuatazo za mofimu.
1.Mofimu ni kipashio chenye maana ya kisarufi.
Ni kweli kuwa mofimu hubeba maana ya kisarufi. Vijisehemu hivi ni muhimu sana katika sarufi.
Kwa mfano, katika neno anacheka tunaweza kupata mofimu zifuatazo.
a-na-chek-w-a
Mofimu Maana ya kisarufi
a nafsi ya tatu umoja
na wakati uliopo
chek mzizi
w kauli/mnyambuliko wa kitenzi
a kauli tenda/kiishio
- Mofimu haiwezi kugawika zaidi
Mofimu tulizoziona hapo juu haziwezi kuvunjwavunjwa zaidi. Zitapoteza maana.
Ni vizuri kutofautisha silabi na mofimu.
Silabi ni kipashio cha utamkaji ilhali mofimu ni kipashio kidogo cha kisarufi chenye maana.
Kwa hivyo,tunapoonyesha mofimu katika neno tuwe makini tusionyeshe silabi.
Tazama neno lifuatalo: Anaimba
Silabi: a+na+i+mbi+wa
Silabi hutamkika,vilevile baadhi ya vijisehemu hivi havina maana ya kisarufi.
Mofimu: a-na-imb-iw-a
Sehemu hizi zina maana ya kisarufi.
Aina mbili kuu za mofimu
- Mofimu huru
- Mofimu tegemezi
Mofimu huru
Mofimu huru hujisimamia kimaana kama neno kamili.Kimsingi hili ni neno kamili kwa sababu lina maana iliyokamilika. Haliwezi kuvunjavunjwa bila kupoteza maana yake.
Mfano: leo,simu,meza,peremende,karatasi,darasa,hukumu,jaji,picha …
TANBIHI: Maneno haya yanaweza kuambishwa na kuwa mofimu tegemezi.
Mfano: jimeza (ji+meza)
Mofimu tegemezi
Hii ni mofimu ambayo hutegemea mofimu nyingine ili kuleta maana inayokusudiwa.
Mfano ;
Mtu : m-tu,wa-tu
Komesha: kom-esh-a
Letwa : let-w-a
Majukumu ya mofimu katika neno
- Mzizi wa neno
Mzizi unaweza kuwa huru au funge
Mzizi huru: sahau,dharau,safiri
Mzizi funge: fung,pik,som,chek,l,ny,ch
- Nafsi
NAFSI |
UMOJA |
WINGI |
vitenzi |
Ya kwanza |
NI |
TU |
ni-na-ok-a, tu-na-ok-a |
Ya pili |
U |
M |
u-na-ok-a, m-na-ok-a |
Ya tatu |
A |
WA |
a-na-ok-a, wa-na-ok-a |
- Ngeli
a-na-li-a : a-ngeli ya A-WA
li-me-fik-a: li-ngali ya LI-YA
- Umoja na wingi
m-tu: m-umoja
wa-tu: wa-wingi
ma-toto: ma-wingi
- Hali
Me-hali timilifu-amechoka
Hu- hali ya mazoea-hucheza
a-Hali isiyodhihirika-akamatwa
po- hali ya mazoea/wakati wowote- asomapo
ki-hali ya masharti- akija
- Yambwa (mtendwa/shamirisho kipozi, mtendewa/yambiwa/shamirisho kitondo)
Ku- nitakuonyesha
m-nitampigia
wa-nitawakomesha
- Mahali
Po- aliposimama (matumizi ya po mara nyingi hujitokeza kimuktadha)
Ni –kanisani,dukani,bungeni
Ko-alikoingia
Mo-alimoingia
- Kiulizi
Wasemaje?
- Amri
Ni- someni,simameni,tokeni
- Kauli/mnyambuliko
Mofimu za kauli za vitenzi ni nyingi sana katika lugha ya Kiswahili.
Kwa mfano:
a-Kauli tenda: fik-a
w-kauli tendwa: som-w-a
liw-kauli tendewa: kagu-liw-a
ek-kauli tendeka: pik-ik-a
esh-kauli tendesha: wez-esh-a
- Vikanushi
Ku-kikanushi cha wa wakati uliopita : hakusoma
Ja-kikanushi cha hali timilifu: hajakuona
Si-kikanushi cha nafsi ya kwanza: siendi
Hu-kikanushi cha nafsi ya pili: huendi
Ha-kikanushi cha nafsi ya tatu: haendi
Namna ya kutambua mofimu za kukanusha
Andika neno katika hali yakinifu kisha ulikanushe
Anasoma- hasomi
Amesoma-hajasoma
Alisoma-hakusoma
- Kijalizo
Ku-alikuja
- Kiishio/kauli tenda
A:chek-a
- Ukubwa na udogo wa nomino
Ki-udogo: kitoto
Ji-ukubwa:jitoto
Maswali
- Eleza maana ya mofimu. (alama 1)
- Tofautisha mofimu na kiambishi. (alama 1)
- Tofautisha mofimu huru na mofimu tegemezi. (alama 2)
- Toa mifano miwili ya mofimu huru. (alama 1)
- Bainisha mofimu katika neno lifuatalo; (alama 3) Hatujajibiwa