Alama za uakifishaji hutumika katika maandishi ili kufafanua maana, kutenganisha mawazo, na kupanga sentensi. Zinasaidia wasomi kuelewa jinsi sentensi inavyopaswa kusomwa, kama ni swali, taarifa, au mshangao, na kutoa mapumziko au msisitizo inapohitajika. Baadhi ya alama za uakifishaji zinazotumiwa sana ni kama vile:
- Nukta (.)
- Koma (,)
- Kiulizi(?)
- Alama ya mshangao (!)
- Koloni (:)
- semikoloni (;)
- Alama za kunukuu (“ ”)
- kibainishi (’)
- Mabano ( )
- kistari kifupi (-)
- alama za dukuku (…)
Alama za uakifishaji zinasaidia kupanga maandishi na kuhakikisha kwamba maana inayokusudiwa inafikishwa wazi kwa msomi/msikilizaji.
Alama za mtajo/usemi (” ”)
a) Usemi Halisi
“Njoo kesho,” mama akamwambia.
b) Lugha Geni/Neno la Kukopwa
“Ninunulie ‘Indomie’ ukifikia sokoni.
c) Kuandika Anwani za Filamu,
“Vioja Mahakamani”
Nukta za Dukuduku (…):
a) Kuonyesha maneno yameachwa
Haraka haraka…
b) Kukatizwa usemi/kauli
Mama: Umesema…
Mtoto: Nimesema nitarudi jioni.
Koma/Mkato/Kipumuo (,):
a) Pumziko fupi katika sentensi
Je, utarudi leo?
b) Kuorodhesha
Alinunua mboga, samaki, nyanya, na viazi.
c)Katika Usemi Halisi
“Nitachelewa,” mama akamwambia.
d) Kuandika Anwani
Wizara ya Elimu,
S.L.P 10,
Naoirobi.
e) Kuandika Tarehe
Alibatizwa mwezi wa Julai, tarehe 20, 2007.
Ritifaa/Kibainishi (’):
a)Herufi imeachwa
Wal’otutuma
b)Shadda/Mkazo
‘iba, ka’lamu
c) Sauti ya King’ong’o
Ng`ombe amekufa.
Mshazari/Mkwaju (/):
a) Tarehe
Alizaliwa tarehe 5/6/1998.
b) Kuonyesha Kumbukumbu
KUMB 1/2024
c) Kuonyesha Visawe
Nenda katika shule/skuli.
d) Kuonyesha “Au”
Wazazi/walezi wamearikwa.
Kistari kifupi (-):
a)Kuandika Tarehe
5-6-2013
b)Kutenga Silabi
a-la-ye
c) Hadi/Kipindi cha Tukio Fulani
1999-2008
d) Kutenganisha Usemi na Msemaji
Lazima tufanye kazi kwa bidii-Kibaki
Kistari Kirefu (–):
a) Kutoa Maelezo Zaidi
Nchi za Afrika Mashariki – Kenyana Tanzania – zinatumia Kiswahili kama lugha ya kitaifa.
c) Kuonyesha Msemaji wa Kauli Fulani
Umoja ni nguvu – Nyerere.
Kikomo/Kitone/Nukta (.):
a) Mwisho wa Sentensi
Atafika kesho.
b) Kuandika Tarehe
12.5.2021
Kuonyesha Ufupisho wa Maneno
Dkt., Bw.,
Kutenga Shilingi na Senti
10.20 – Shilingi kumi na senti ishirini
Nusu/Semi Koloni/Nukta Mkato (;):
a) Kugawa Sentensi Bila Viunganishi
Amekulete zawadi nyingi; hazijakufurahisha.
Kama Kipumziko Katika Sentensi Ndefu
Baada ya kuchunguza hati aliyopewa na wafanyabiashara hao, aligundua haikuwa nzuri; hivyo akaamua kujiondoa nayo.
Vifungo/Mabano/Paradesi ( ):
a) Kuonyesha Maelezo ya Vitendo vya Msemaji/maleezo ya jukwaa
Fatuma: (Akicheka.) Umeshiba kweli!
b) Kutoa Maelezo Zaidi
Amin(alituzwa na rais) amepandishwa cheo.
Herufi Kubwa (H):
Mwanzoni mwa Sentensi
“Twendeni zetu,” akatwambia.
Baada ya alama hisi katika sentensi hisishi.
- Salale! Umepoteza pesa zote.
Mwanzoni mwa Nomino za Pekee
Hadija, Kenya, Uganda, Jumamosi
Ufupisho wa Maneno
C.C.M (Chama cha Mapinduzi)
Koloni/Nukta Mbili (:)
a) Kuonyesha Orodha
Ili kuandaa samosa, unahitaji viungo vifuatavyo: unga, nyama, chumvi, mafuta, na kitunguu.
b) Kuandika Mazungumzo
Rhoda: Umekawia wapi?
c) Kutenganisha Saa na Dakika
7:45
Hisi/Mshangao (!):
Kuamrisha
Kachezeeni nje!
Baada ya Vihisishi
Masalaale! Pesa zangu zote zimeibwa.
Kiulizo (?):
Mwisho wa Sentensi ya ulizi
Umetoka wapi?
Herufi Nzito (h):
Kusisitiza
Jibu maswali manne pekee.
Herufi za Mlazo/Italiki (h):
Kuonyesha Neno la Kigeni
Tumealikwa na President.
Kinyota (*):
Kuonyesha neno fulani limeendelezwa Vibaya
Nipe shilingi *isirini.