Dhana ya mzizi wa neno

mfano wa mzizi
Tunaposikia neno mzizi jambo la kwanza ambalo hutujia akilini ni sehemu fulani ya mti.Mti husimama na kukua kwa sababu umeshikiliwa ardhini na mizizi.Hivyo basi,neno huitaji mzizi.
Sehemu hii ni muhimu sana katika neno kwani hubeba maana ya kimsingi ya neno fulani.Kwa mfano kutokana na mzizi –tu tunaweza kupata maneno kama; mtu,watu,kitu,vitu. Kwa hivyo, mzizi hutumiwa tunapounda maneno katika lugha.Sehemu hii pia haibadiliki hata neno likiongezwa viambishi.
Kwa mfano:
- Wanaochekwa,tuliowacheka (mzizi ni chek)
- Vilivyosomwa,someana,somesha,somwa
Kutokana na mifano hii tunaweza kusema mzizi ni sehemu ya neno ambayo huongezwa viambishi au sehemu ambayo hubakia baada ya kuondoa viambishi awali na tamati.
Kutambua mzizi katika neno
Jambo la kwanza ni kuondoa viambishi.
Kwa mfano: waliangukia
Wa-li-anguk-i-a ,mzizi ni anguk
Aina za mzizi
Katika lugha ya Kiswahili kuna mzizi huru na mzizi funge.Mzizi huru huwa neno kamili bila kuongezwa viambishi.Kwa mfano,leo,kamusi,sahau,dharau.. Mzizi funge huongezwa viambishi ili kuwa na maana kamili,kwa mfano anguk,som,on,pig,andik,f,l,ch, …
Maswali
Onyesha mzizi katika maneno yafuatayo
- nywishiana
- Alinijia
- Pakuliwa
- Oneana
- Safirishiwa
- Valiana
- pokezwa