Viambishi Maalumu
Viambishi maalumu huwa na matumizi ya kipekee katika neno au sentensi. Hapa chini tutachambua aina za viambishi maalumu na mifano yake.
1. Kiambishi ‘ni’
- a) Nafsi ya kwanza umoja
Nitafika kesho - b) Mahali
Ameenda nyumabni. - c) Kitenzi kishirikishi kipungufu
Yeye ni daktari. - d) Wingi
Tokeni nje.
2. Kiambishi ‘ndi’
- Kitenzi kishirikishi kipungufu
Yeye ndiye aliniibia pesa.
3. Kiambishi ‘ji’
- a) Udogo
Kitoto kinalia. - b) Ukubwa
Jibwa limebweka. - c) Kirejeshi cha mtenda
Alijikata makono. - d) Nafsi ya pili
Jinunulie upendacho. - e) Kiambishi tamati cha kuundia nomino
Mwimbaji alituzwa na mgeni wa heshima.
4. Kiambishi ‘Ki’
- a) Kitendo ki katika hali ya kuendelea
Tulikuwa tukila alipoingia. - b) Masharti/Kitendo kinategemea kingine
Utapita mtihani ukijitahidi. - c) Udogo wa nomino
Kitoto kinalia. - d) Ngeli
Kiti kimevunjika. - e) Kitenzi kishirikishi kipungufu
Chakula ki mezani. - f) Kielezi namna mfanano
Yeye hutembea kijeshi. - g) Kitendo hakifanyiki kamwe
Kitabu hiki hakisomeki.
5. Kiambishi ‘ku’
- a) Kikanushi cha wakati uliopita
Hakunialika. - b) Nafsi ya pili umoja
Alikupigia simu jana. - c) Mahali kusikodhihirika
Huko kungepakwa rangi. - d) Ngeli
Kusoma kwake kunapendeza.
6. Kiambishi ‘ka’
- a) Mfuatano wa matukio
Tulikula chakula, tukanywa chai kisha tukalala. - b) Vichwa vya habari
Mwizi kapigwa mawe. - c) Kutoa amri
Kachezeeni nje! - d) Kitendo fulani ni tokeo la kingine
Tulisoma kwa bidii tukapita mtihani. - e) Kutoa nasaha/kushauri
Kamwombe Mola baraka.
7. Kiambishi ‘a’
- a) Hali isiyodhihirika
Rais wa Marekaniawasili nchini. - b) Vichwa vya habari
Waziri azomewa na wananchi. - c) Kitendo kinaendelea
Twasoma magazeti. - d) Nafsi ya tatu umoja
Yeye atafaulu sana. - e) Ngeli ya A-WA
Twiga anapendeza sana. - f) Kiishio/kauli tenda katika vitenzi
Anacheza.
8. Kiambishi ‘nge/ngali’ (Masharti Yanayowezekana au Yasiyowezekana)
- Mfano wa masharti yanayowezekana
Ningekuwa na pesa, ningenunua kiatu. - Mfano wa masharti yasiyowezekana
Laiti ningalijua nisingaliingia katika hilo basi.
9. Kiambishi ‘po’
- a) Mahali
Nionyeshe alipoketi. - b) Wakati maalumu
- Anapotokea wanyama hutoroka.
10. Kiambishi ‘kwa’
- a) Mahali
Ameenda kwa Shangazi. - b) Jinsi
Alisoma kwa bidii. - c) Sehemu ya kitu
Amepata alama moja kwa tano katika mtihani. - d) Pamoja na
Mkutano ulijaa wazee kwa vijana. - e) Kuonyesha kitu kilitumiwa kama kifaa
Alikata mkate kwa kisu. - f) Sababu
Aliugua kwa kunywa maji machafu. - h) Muda / Kipindi
Alilia kwa nusu sana.
Maneno Maalumu
Maneno maalumu ni maneno ambayo huwa na matumizi maalumu katika sentensi. Hapa chini, tutachambua maneno maalumu na matumizi yake.
1. Ila
- a) Isipokuwa
Watu wote ila yeye wameenda. - b) Kasoro
Hakuna kizuri kisicho na ila.
2. Labda (Pengine / Shaka)
Mfano: Haonekani siku hizi, labda amepata uhamisho.
3. Ikiwa
- a) (Kama / Shaka)
Tutamkuta nyumbani ikiwa amepewa likizo. - b) Masharti
Mgonjwa atapona ikiwa atakunywa dawa ipasavyo.
4. Walakini
- a) Dosari
Gari limekamatwa kwa sababu lilikuwa na walakini. - b) Lakini / Bali
Amelipa bali hajauziwa.
5. Ingawa / Ingawaje (Hata Kama)
Mfano: Nilienda kazini ingawa sikuwa na nauli.
6. Ijapokuwa / Ijapo / Japo (Hata Kama)
Mfano: Usicheze na nyoka ijapokuwa ni mdogo.
7. Jinsi
a) aina/namna/sampuli
Siwezi kula chakula jinsi hii.
b) kulingana na/kama
Alinilipa jinsi ulivyomwambia
8. Na
- a) Kiunganishi
Mama na baba wanalima. - b) Umilikaji
Rhoda ana kitabu kizuri. - c) Wakati Uliopo
Anaandika barua. - d) Kauli / Mnyambuliko
Pate na Simba wanaandikiana barua. - e) Kuonyesha Tofauti
Kiatu hiki ni tofauti na kile.
Hitimisho
Kwa kuelewa matumizi ya viambishi maalumu na maneno maalumu, utaweza kuboresha ufanisi wa matumizi ya lugha ya Kiswahili chako. Endelea kujifunza na kutumia mifano hii ili kuboresha ufanisi wa mawasiliano yako katika Kiswahili!