Said A.Mohamed ni mwandishi mwenyee umaarufu mkubwa katika Fasihi ya Kiswahili. Vitabu vyake huwavutia wasomaji sana.
Hadithi fupi huwaiwaitaji wasomaji wawe makini sana ili waelewe kinachozungumziwa na maudhui. Wanufunzi hukosa mifano faafu na ya kutosha katika hadithi fupi.
Tumbo Lisiloshiba-Said A. Mohamed
Tamaa ni hamu kubwa ya kupata kitu. Mtu aliye
na tamaa ni mtu ambaye hatosheki. Kutokana na maana hii tunaweza kusema kuwa
mtu mwenye tumbo lisiloshiba ni mtu mwenye tamaa kwa sababu anakula na
hatosheki.
Ikumbukwe kuwa anwani Tumbo
Lisiloshiba imetumika kijazanda ikiwa na
maana ya watu (wenye mali) ambao hawatosheki, wana hamu kubwa ya kupata mali
zaidi.
Jitu la miraba minne lina tamaa ya chakula.Linapoingia katika mkahawa mshenzi kwa Mzee Mago linaitisha na kula chakula chote.
Kabla ya kuendeleza mjadala huu ningependa
nirejelee maneno yafuatayo (tunawasaidia Wanamadongoporomoka kutegua
kitendawili);
- “Wala sitaki msaada wako dhaifu”
Kwa hivyo jitu hili linatumbua kuwa “msaada” wa Mzee Mago ni dhaifu, Mzee Mago anaishi Madongoporomoka “ wanakoishi watu wepesi wasio na mashiko”.
- “ Nimekuja kukusaidia wewe.
Nitakusaidia sana. Usiwe na wasiwasi”
Maneno haya ni kinaya. Jitu lenye tumbo lisiloshiba linamhakikishia Mzee Mago kuwa linakuja kula ardhi yake. Polisi wanatumiwa na watu wa aina hii kuwafukuza na kuwapiga wananchi wasio na hatia ili wahame katika ardhi yao.Wahame? Hapana, hawana pa kuhamia,jiji limejaa “ tukiondoshwa hapa tutakwenda wapi hapa jijini?”- maneno ya Kabwe.Watu walio nacho wanaongozwa na tamaa kwa hivyo hawawezi kuwasaidia maskini wanaoishi Madongoporomoka.
- “Wakikubali wasikubali,itabidi leo
chakula chote nikile mimi”
Wanamadongoporomoka wakubali
wasikubali ardhi ya watu wasio na nguvu itanyakuliwa. Linakula chakula chote
hata cha wale waliokuwa wamepanga kula hapo mkahawani.Tunatambua kuwa ardhi
inayonyakuliwa, inanyakuliwa kwa lazima na watu wenye tamaa na wenyewe hawana
pa kwenda “ hawajui wakimbilie wapi”
Jitu hili lina tamaa, ni
kweli kwa sababu lina mipango ya kunyakua ardhi ya watu wengi ambao hawana
kwingine, hii si ni njaa kubwa ajabu?
- “Nitalipa gharama zote. Nitalipa
mara tatu tu …”
Tunatambua kuwa Jitu hili ni bwanyenye. Ni tamaa tu inaliongoza.Lina uwezo wa kulipa chakula chote ambacho kingewalisha watu wengi tena mara tatu. Lina mali nyingi lakini halitosheki.
- “Kesho kama sote tutaamka salama”
Maneno haya ni kinaya. Kila
mtu aliamshwa na vishindo na vitisho vya mabuldoza na waliokuwa wamelala
kutimuliwa na askari wa baraza.Jitu nalo lilifika kwa gari kubwa huku
likitabasamu.
- “ kama tutafungua milango ya
nyumba zetu zinazosimama juu ya ardhi hii adhimu..”
Anawakejeli
Wanamadongoporomka. Wengi hawakuweza kufungua milango yao ya vibanda
mshenzi ,vinabomolewa na askari wa baraza la mji. Je,ardhi hii ni
ardhimu? Ardhi ambayo itahitaji kusafishwa, kukogeshwa na kusuuzwa?
- “Nimekuja kula ardhi yako leo”
Ikumbukwe kuwa jitu
likiondoka liliagiza kuwekewa chakula mara mbili. Kutokana na maneno haya
tunatambua kuwa limefika kuhakikisha Wanamadongoporomoka wamefukuzwa ili liweze
kumiliki ardhi yote.Hii ni tamaa.
Jitu hili lina tamaa ya kujiongezea mali. Jijini kumejazwa majumba na wakubwa mpaka hakuna nafasi hata ya mtu kuvuta pumzi.
Jitu hili kweli halishibi linaendelea kula tu,
lina tamaa ya kuendelea kumiliki mali zaidi. Baada ya kulijaza jiji wakubwa
wanataka kunyakua ardhi ya Wanamadongoporomoka.
Wakubwa wana tamaa kubwa, wanataka kuchukua ardhi ya watu maskini kwa lazima. Ardhi ya Wanamadongoporomoka inachukuliwa kwa lazima,askari wa baraza wanabomoa vibanda,kupiga na kuwafukuza watu huku wamelindwa na jeshi la polisi lilokuwa limebeba bunduki.
Lakini fujo hizi hazikuwahamisha Wanamadongoporomoka
Kutokana na uzito wa maudhui ya tamaa mifano iliyotolewa hapa au itakayotelewa inaweza kutumika kuelezea ufaafu wa anwani.