Silabi ni kipashio kinachotamkika
Maana
Sauti mbili au zaidi zinazotamkwa kwa pamoja.
Sauti mbili au zaidi ambazo hutamkwa kama fungu moja la sauti.
Aina za silabi
Kuna aina mbili za sila katika Kiswahili
Silabi funge
Hizi ni silabi ambazo huishwa kwa konsonanti
Mfano: m-tu
Silabi wazi/huru
Hizi ni silabi ambazo huishia kwa irabu
Mfano: ka-ka, le-o,u-si-ku
MUUNDO WA SILABI
Kuna miundo mbalimbali ya silabi katika Kiswahil
Irabu pekee
o-a,i-ta
konsonanti pekee
m-tu
konsonanti irabu
ji-tu
konsonanti konsonanti irabu
fye-ka, bwe-ka
konsonanti konsonanti konsonanti irabu
mbwe-ha,twa-ngwa
Mifano ya maswali
- Eleza maana ya silabi.(alama 1)
- Huku ukitoa mifano eleza aina mbili za silabi. (alama 2)
- Eleza miundo yoyote miwili ya silabi. (alama 2)
- Tenganisha silabi: viyeyusho (alama 2)
- Tunga neno lenye muundo ufuatao: KI+KI+I. (alama 2)
