Top 10 Swahili proverbs
- Haraka haraka haina Baraka
- Ukifanya jambo kwa haraka huenda usifanikiwe
- Mke ni nguo mgomba ni kupalilia
- Kitu kizuri huwa kimetunzwa vizuri
- Chelewa chelewa utapata mwana si wako
- Mtu ambaye huwa wa kwanza katika jambo huweza kupata kitu kizuri
- Masikini akipata matako hulia mbwata
- Mtu ambaye alikuwa mhitaji akifanikiwa huanza kuwa na maringo
- Adui wa mtu ni mtu
- Adui wa mtu ni mtu
- Maskini haokoti akiokota huambiwa kaiba
- Mtu ambaye ni maskini hukosa mafanikio katika mambo mengi maishani
- Ukistaajabu ya Musa utayaona ya
firauni
- Ukishangazwa na jambo moja kuna jambo jingine kubwa zaidi na litakushangaza zaidi
- Angurumapo samba mcheza nani?
- Mtu mwenye uwezo/mamlaka akiongoea wengine hunyamaza
- Akili nyingi huondoa maarifa
- Iwapo mtu anajiona mwerevu sana huenda akaanza kufanya upumbavu
- Akili ni nywele kila mtu ana zake
- Kila mtu ana uwezo/busara/maarifa ya kufanya jambo Fulani
- Mgeni njoo mwenyeji apone
- Mgeni ni Baraka kwa mwenyeji
- Siku za mwizi ni arubaini
- Maovu huwa na mwisho wake
- Mwizi akishikwa husema kaokota
- Mtu akifanya jambo baya hutafuta kisingizio ili kujitetea
- Mgema akisifiwa tembo hulitia maji
- Sifa nyingi zinaweza kumpotosha mtu
- Usimwage mtama kwenye kuku wengi
- Usiwe na tabia ya kutoa siri zako mbele ya watu wengi
- Wema hauozi
- Matendo mazuri huleta faida
- Ngoja ngoja huumiza matumbo
- Kuchelewa kutekeleza jambo Fulani husababisha madhara
- Siku ya nyani kufa miti yote huteleza
- Ujanja/unafiki/Maovu ambayo mtu amekuwa akifanya siku ya kugunduliwa ikifika hana pa kujificha
- Kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa
kusonga ugali.
- Ata ukipatwa na changamoto maishani usife moyo
- Maji ukiyavulia nguo huna budi
kuyaoga
- Ukifanya jambo baya itakubidi ukubali matokeo yake
