KISWAHILI
Karatasi ya 1
INSHA Okt/Nov, 2008
Karatasi ya 1
INSHA
Maagizo
- Andika
Insha mbili insha ya kwanza ni ya lazima.
- Kisha
chagua insha moja nyingine kutoka hizo tatu zilizobakia.
- Kila
insha isipungue maneno 400.
- Kila
insha ina alama 20.
- Insha
ya lazima.
- Andika tahariri kwa gazeti la Raia ukieleza hatua zinazochukuliwa nchini ilikumwendeleza kielimu mtoto msichana.
- “Ufisadi
ndicho kikwazo kikuu katika maendeleo ya uchumi wa taifa lolote.”
Thibitisha.
- Matikiti na matango ndiyo maponya njaa.
- Andika insha itakayomalizikia kwa ; “Aha! Kumbe mwungana akivuliwa nguo huchutama. Sitaisahau siku hiyo kwani sijawahi kufedheheka maishani kama nilivyoaibika siku hiyo
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA
Swali La Kwanza
Tahariri Kwa Gazeti La Raia
a) Sura
- Iwe na kichwa.
- Iwe na tarehe.
- Iwe na
utangulizi.
- Iwe na
mwili/maelezo kiaya.
- Yaweza kuwa na
maoni au msimamo wa mhariri au msimamo wa gazeti.
- Iwe na
hitimisho k.m. jina la mhariri na wadhifa wake.
b) Maudhui: Kuendeleza Msichana Kielimu
- Kupiga vita ndoa
za mapema.
- Kupiga marufuku
ajira ya watoto.
- Wasichana
wapewe nafasi ya kuendelea na masomo ya baada kujifungua.
- Alama za
kujuinga na shule na vyuo vikuu kupunguzwe kwa wasichana.
- Elimu bila
malipo kwa watoto wa shule za msingi na za upili.
- Kutoa msaada wa
karo kwa familia maskini.
- Kujenga shule
zaidi za wasichana.
- Mashirika yasiyo
ya kiserikali kujenga shule na vyuo.
- Kuhamasisha wazazi
kuhusu umuhimu wa elimu ya mtoto msichana.
- Adhabu kali kwa
wabakaji. (Alama
20)
Swali La Pili:
a) Ufisadi Kama Kikwazo
- Hii ni insha ya
hoja.
- Hoja ziunge mkono
kauli hii.
- Mtahiniwa
akubaliane na kauli hii.
- Mtahiniwa ahusishe
ufisadi unavyodumaza uchumi wa nchi.
b) Hoja
- Watu kupewa
kazi wasizoweza.
- Wanaostahili
kazi hawapati.
- Biashara haramu
huwapunja raia.
- Wawekezaji
huvunjwa moyo.
- Miradi ya
maendeleo kukwama/kutomalizwa.
- Baadhi ya maeneo
ya nchi kupuuzwa kimaendelepo.
- Nchi kukosa
misaada.
- Taifa hutumia pesa
nyingi kurekebisha ufisadi.
- Sifa za nchi
kuharibika.
- uhalifu
kuenea/kukosa usalama.
Swali La Tatu
a) Methali: “Matikiti Na Matango Ndiyo
Maponya Njaa”
- Hii ni methali.
- Mtahiniwa atunge
kisa/visa kuonyesha ukweli wa methali hii.
- Kisa kionyeshe
sehemu mbili za methali.
- Upuuzaji/kudunisha kitu, jambo au mtu.
- Kitu, mtu au jambo hilo lije liwe ni la manufaa baadaye
wakati wa shida.
b) Msamiati wa methali
- Matikiti na
matango = aina ya vyakula visivyothaminiwa sana.
- Maponya =
yanayookoa/yanayofaa
- Njaa = shida
c) Maana ya methali
Vitu
tunavyodunisha/tunavyopuuza huweza kuwa na msaada mkubwa wakati wa shida. Kitu tulichonacho mkononi mwetu ndicho
kinaweza kututoa taabani wakati wa shida, hivyo basi tusikidharau.
Swali La Nne
a) Insha Ya Mdokezo
- Hii ni Insha ya
mdokezo na mdokezo huu ni wa kumalizia.
- Mtahiniwa atunge
kisa kinachomalizikia kwa dondoo hili.
- Mtahiniwa
ajihusishe katika kisa hiki.
- Mtahiniwa
atumie nafsi ya kwanza
- Kisa kiwe na
tendo/jambo baya kisiri
- Jambo hili
linawekwa wazi
- Mhusika anakosa
uso yaani anaaibika sana.
b) Methali: “Muungwana
akivuliwa nguo huchutama”.
Maana: Uovu wa mtu anayedhaminiwa ni mwema unapofishuliwa yeye huaibika.