“Jamii imemkandamiza mwanamke.“
Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea Tamthilia ya Kigogo.
1. Kudharauliwa
Majoka anasema wanawake ni wanawake tu.
2. Kutumiwa kama chombo cha mapenzi
Majoka anataka kuishiriki mapenzi na Ashua kama kigezo cha kumpa msaada.
3. Kupigwa
Tunu anapigwa na kuvunjwa mguu na Chopi,Ngurumo na vijana wengine.
4. Kutusiwa
Majoka anasema « sina time ya wanawake »
5. Kufungwa bila hatia
Majoka anamfunga Ashua kwa madai ya kuzua vurugu katika ofisi ya serikali.Ilikuwa ni njia ya kulipiza kisasi kwa Sudi na kumnasa Ashua.
6. Kunyimwa kura
Tunu anapoenda mangweni kujaribu kuwakomboa walevi wamuimbia nyimbo za kumkejeli. Ngurumu anadai kuwa hawezi kumpa mwanamke kura.
7. Kutopewa nafasi ya uongozi katika jamii
Kenga anamwuliza Sudi iwapo Sagamayo ishawahi kuwa na Shujaa wa kike.
8. Kupangiwa njama ya kuuwawa
Kenga na Majoka wanapanga njama ya kumwangamiza Tunu.Wanawatuma vijana,akiwepo Chopi kumwangamiza lakini wanamvunja mguu.
9. Kuishi kwa hofu
Hashima anasema kuwa yeye na Tunu wake wanaishi kwa hofu,kila waamkapo wanapiga alhamdulillahi.
10. Kusalitiwa katika ndoa
Majoka anasema kuwa hampendi Husda bali alimwoa ili kutimiza wajibu wake kama kiongozi.Majoka anampenda Ashua.
