Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Hapa duniani, moyo unaimba
Mioyo yetu yakutane, furaha tutaona
Pamoja, tusimame, tukishirikiana
Nchi yetu tukuzwe, kwa upendo tuunganishe.
Mawingu yananing’aa, jua likiangaza
Safari yetu ya maisha, kila siku ni zawadi
Kwa upendo na matumaini, tutaendelea mbele
Kupitia changamoto zote, tutashinda kwa pamoja.
Nchi yetu, yenye utajiri ,wa asili na tamaduni
Sijali rangi, lugha, au dini tunazofuata
Kwa umoja na amani, tuwe kitu kimoja
Tuwepo kwa wenzetu, kwa kila mtu, tuwapende.
Kwa Swahili yetu, tulinde na tuhifadhi
Historia yetu, tunayoipenda na kujivunia
Tukumbuke waliotangulia, na kuwaongoza vizazi vyetu
Nchi yetu, taifa letu, kwa daima tutakuwa pamoja.
Maswali
a) Pendekeza kichwa cha shairi hili. (alama 1)
b) Tambua aina ya shairi hili. (alama 2)
c) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
d) Fafanua Bahari katika shairi hili kwa kurejelea idadi ya mishororo. (alama 1)
e) Tambua mbinu zozote mbili ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi. (alama 2)
f) Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 1)
g) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)
h) Tambua mbinu mbili za kimtindo zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
i) Onyesha aina za urudiaji zinazojitokea katika shairi hili. (alama 2)
j) Tambua nafsi neni katika shairi hili. (alama 1)
Majibu
a)Pendekeza kichwa cha shairi hili. (alama 1)
Tuipende nchi yetu
b)Tambua aina ya shairi hili. (alama 2)
Shiri huru- idadi ya vipande katika mishororo hailingani
c)Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
-Lina beti nne
-Kila ubeti una mishororo minne
-Idadi ya vina ni tofauti katika baadhi ya mishororo
-Idadi ya vipande ni tofauti katika baadhi ya mishororo.
d)Fafanua Bahari katika shairi hili kwa kurejelea idadi ya mishororo. (alama 1)
– Tarbia- kila ubeti una mishororo minne
c)Tambua mbinu zozote mbili ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi. (alama 2)
-Kuboronga sarufi- “hapa duniani moyo unaimba” badala ya “moyo unaimba hapa duniani”
-Inkisari- sijali badala ya usijali/tusijali
d)Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 1)
Anawahamasisha wananchi kuishi kwa umoja, kuwa na matumaini, upendo na kuhifadhi historia yao.
e)Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)
Nchi yetu ina utajiri wa asili na tamaduni. Tusijali rangi, lugha, au dini tunazofuata. Kwa umoja na amani tuwe kitu kimoja. Tuwepo kwa wenzetu na tuwapende.
f)Tambua mbinu mbili za kimtindo zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
-Uhaishaji- moyo unaimba
-Stiari- safari yetu ya maisha ni zawadi
g)Onyesha aina za urudiaji zinazojitokea katika shairi hili. (alama 2)
-Urudiaji wa neno- yetu
-Urudiaji wa kifungu cha maneno- nchi yetu
h)Tambua nafsi neni katika shairi hili. (alama 1)
Mzalendo/mtu anayeipenda nchi yake- Nchi yetu, taifa letu, kwa daima tutakuwa pamoja.