Ngeli ni mpangilio wa nomino katika makundi. Mpangilio huu ni muhimu sana katika lugha ya Kiswahili kwani husaidia katika upatanisho wa nomino na vitenzi na maneno mengine. Mbinu hii huitwa upatanisho wa kisarufi.
Ngeli za Kiswahili |
---|
A-WA |
LI-YA |
U-ZI |
U-I |
KI-VI |
U-U |
I-ZI |
KU |
YA-YA |
I-I |
U-YA |
PA-KU-MU |
A-WA
Ngeli hii hujumuisha majina ya binadamu na viumbe vilivyo hai. Huwa na kiambishi a katika umoja na wa katika wingi.
Kiambishi cha umoja-a
Kiambishi cha wingi-wa
Mfano
Mtoto anacheza.
Watoto wana cheza.
Ndege anaimba .
Ndege wanaimba.
Miundo ya nomino
KI-VI
Kipepeo anapendeza.
Vipepeo wanapendeza.
CH-VY
Chura aliruka.
Vyura waliruka.
M-WA
Mtu ameonekana.
Watu wameonekana.
M-MI
Mtume anahubiri.
Mitume wanahubiri.
Ngeli ya KU
Hii ni ngeli ya kitenzi jina. Vitenzi vinapoongezwa kiambishi ku na kutumiwa kama nomino katika sentensi ,hubadilika na kuwa vitenzi jina. Nomino hii huwa na kiambishi ku katika upatanisho wa kisarufi.
Mfano
Cheka-kucheka
Kucheka kwake kunavutia.
Cheza-kucheza
Kucheza huko hakufai barabarani.
Tanbihi: Lazima kitenzi kitumike kama nomino ili kipiwe sifa hii.
Tazama: Ameanza kucheza. Neno “kucheza” ni kitenzi wala si kitenzi jina.
Ngeli ya I-ZI
Hii ni ngeli ya nomino ambazo huwa katika hali ya umoja.
Kiambishi cha umoja-i
Kiambishi cha wingi-zi
Mfano
Ngozi hiyo inavutia.
Ngozi hizo zinavutia.
Ngeli hiyo inaeleweka.
Ngeli hizo zinaeleweka.
Ngeli ya LI-YA
Kiambishi cha umoja-li
Kiambishi cha wingi-ya
Mfano
Gari limenunuliwa.
Magari yamenunuliwa.
Muindo ya nomino
G-M
Gari-magari
JI-MA
Jani-majani
Jicho-macho
Y-M
Yai –mayai
JI-ME
Jino-meno
Ngeli ya PA-KU-MU
Hii ni ngeli inayoashiria mahali. Kila kiambishi katika ngeli hii huwa na matumizi ya kipekee.
Pa- mahali panapodhihirika
Mahali hapa panavutia.
Mu- mahali ndani
Kanasani homo mna watu wengi.
Ku- mahali kusikodhihirika
Mahali huko kumejaa maji.
Ngeli ya KI-VI
Kiambishi cha umoja-ki
Kiambishi cha wingi-vi
Mfano
Kiti kimenunuliwa.
Viti vimenunuliwa.
Kioo kimevunjika.
Vioo vimevunjika.
Ngeli ya U-ZI
Kiambishi cha umoja- u
Kiambishi cha wingi-zi
Mfano
Uta umekatika.
Nyuta zimekatika.
Miundo ya nomino
U-NYU
Uta-nyuta
Uzi-nyuzi
W-NY
wembe- nyembe
Ngeli ya YA-YA
Nomino katika ngeli hii hupatikana katika hali ya wingi.
Kiambishi cha umoja-ya
Kiambishi cha wingi-ya
Mfano
Maji yamemwagika.
Maji yamemwagika.
Mifano ya nomino: mafuta,mate,manukato,maziwa
Ngeli ya U-I
Kiambishi cha umoja-u
Kiambishi cha wingi- i
Mfano
Mkono unaniuma.
Mikono inaniuma.
Mti umekatwa.
Miti imekatwa.
Mlima unavutia.
Milima inavutia.
Ngeli ya I-I
Nomino nyingi katika ngeli hii ni zile zisizohesabika. Nyingine huwa ni nomino dhahania.
Kiambishi cha umoja-i
Kiambishi cha wingi-i
Mfano
Amani imepatikana.
Amani imepatikana.
Sukari imeloa maji.
Sukari imeloa maji.
Ngeli ya U-U
Hii ni ngeli ambayo hujumuisha nomino dhahania.
Kiambishi cha umoja-u
Kiambishi cha wingi-u
Mfano
Upendo utanifaa.
Upendo utawafaa.
Mifano zaidi ya nomino: uzuri,wema,uovu,ukakamavu
Ngeli ya U-YA
Kiambishi cha umoja-u
Kiambishi cha wingi-ya
Mfano
Ugonjwa umetibiwa.
Magonjwa yametibiwa.
Mifano Zaidi ya nomino: uovu,ubaya,unyoya
Tanbihi: Nomino huwa na kiambishi u katika umoja na ma katika wingi
Good work
Felix mutuku
Good work!
Asante lakini ingefaa zaidi kuongeza mifano tofauti
Naam
Kati nzuri kabisa.Keep the Spiret moving.
Type here..Pongezi kwa kazi wastan
the book is very good
ilinisaidia . GOOD WORK