Mandhari Katika Fasihi
MAANA
Ni sehemu ambapo au mazingira ambako matukio ya hadithi au masimulizi yanafaanyika.
Kazi ya fasihi hujengwa katika mazingira maalum ambayo huitwa mandhari.
UFAFANUZI
- Mandhari katika kazi ya fashi husaidia kuleta hisia iliyokusudiwa.
- Mfano kama msanii anakusudia kuleta hisia ya woga humlazimu kuchukua mandhari ya woga kama msitu mnene, ngurumo za wanyama wakali.
- Huonyesha jamii,mahali,wakati wa kihistoria na hali ya maisha ambambo mwandishi anaandika kazi yake.
- Mandhari ya riwaya ni mapana na yanayoendelezwa kikamilifu kwa sababu riwaya hujihusisha na vipengele vingi vya maisha ambavyo hupatikana katika nyakati na mahali tofauti kama vile
shuleni,mijini,vijijini,ng’ambo….
- Hali mbalimbali pia huweza kujitokeza.kwa mfano, hali ya huzuni, furaha,ufanisi,kupungukiwa,kufiwa…..
- Mandhari husaidia kueleza maudhui na dhamira ya mwandishi.
- Maudhui ya kazi lazima yelenge kipindi cha wakati ambapo kazi imeandikwa
Vipengele vya mandhari
- Wakati wa kutukia kwa matendo
- Kutambulisha wahusika.
- Kuonyesha migogoro.
- Kuonyesha matatizo ya kijamii- ulevi,ufisadi,wizi.
- Kueleza mahali pa tukio.
- Kuonyesha taharuki.
- Kuonyesha maudhui
- Kuonyesha hali- hali ya huzuni.
- Kuonyesha kipindi cha wakati-wakati wa ukoloni
- Kuonyesha utamaduni wa jamii
- Kulinganua hali za matabaka.
- Kuonyesha hali ya kiuchumi- je kuna mgao sawa wa mali
SWALI
“ Najihisi kama Kurwa katika novella ya Kurwa na Doto”
Eleza umuhimu wa nafsineni katika kufanikisha mandhari katika riwaya ya Chozi la Heri.
JIBU
- Mandhari huashiria mahali – kupitia mhusika umu tunaona anasomea shule ya tangamano pamoja na wanafunzi wenzake.
- Mandhari huashiria wakati – kupitia umu tunapata wasichana wanne bwenini wakielezana matatizo
- Mandhari huashiria wahusika – kupitia umu tunaona utepetevu wa askari kazini
- Mandhari huchimuza maudhui – kuptia umu tunapata maudhui ya changamoto za malezi anapoachwa na wanuna wake katika mlima wa simba
- Mandhari huibua taharuki – umu anatuonyesha kwao kulikuwa mlima wa simba babake alikozikwa hatujui kama waliwahi rudi huko tena
- Mandhari huonyesha hali – kupitia umu tunapata hali ya masikitiko wanayopitia wanafunzi pale shule ya Tangamano
- Mandhari huashiri tabaka – kupitia mandhari ya nyumbani mwa mwnageka anakopangwa umu kunaashiria tabaka la juu