KISWAHILI
Karatasi ya 1 INSHA Okt/Nov, 2008
Karatasi ya 1
INSHA
Maagizo
- Andika Insha mbili insha ya kwanza ni ya lazima.
- Kisha chagua insha moja nyingine kutoka hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- Insha ya lazima.
- Andika tahariri kwa gazeti la Raia ukieleza hatua zinazochukuliwa nchini ilikumwendeleza kielimu mtoto msichana.
- “Ufisadi ndicho kikwazo kikuu katika maendeleo ya uchumi wa taifa lolote.” Thibitisha.
- Matikiti na matango ndiyo maponya njaa.
- Andika insha itakayomalizikia kwa ; “Aha! Kumbe mwungana akivuliwa nguo huchutama. Sitaisahau siku hiyo kwani sijawahi kufedheheka maishani kama nilivyoaibika siku hiyo
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA
Swali La Kwanza
Tahariri Kwa Gazeti La Raia
a) Sura
- Iwe na kichwa.
- Iwe na tarehe.
- Iwe na utangulizi.
- Iwe na mwili/maelezo kiaya.
- Yaweza kuwa na maoni au msimamo wa mhariri au msimamo wa gazeti.
- Iwe na hitimisho k.m. jina la mhariri na wadhifa wake.
b) Maudhui: Kuendeleza Msichana Kielimu
- Kupiga vita ndoa za mapema.
- Kupiga marufuku ajira ya watoto.
- Wasichana wapewe nafasi ya kuendelea na masomo ya baada kujifungua.
- Alama za kujuinga na shule na vyuo vikuu kupunguzwe kwa wasichana.
- Elimu bila malipo kwa watoto wa shule za msingi na za upili.
- Kutoa msaada wa karo kwa familia maskini.
- Kujenga shule zaidi za wasichana.
- Mashirika yasiyo ya kiserikali kujenga shule na vyuo.
- Kuhamasisha wazazi kuhusu umuhimu wa elimu ya mtoto msichana.
- Adhabu kali kwa wabakaji. (Alama 20)
Swali La Pili:
a) Ufisadi Kama Kikwazo
- Hii ni insha ya hoja.
- Hoja ziunge mkono kauli hii.
- Mtahiniwa akubaliane na kauli hii.
- Mtahiniwa ahusishe ufisadi unavyodumaza uchumi wa nchi.
b) Hoja
- Watu kupewa kazi wasizoweza.
- Wanaostahili kazi hawapati.
- Biashara haramu huwapunja raia.
- Wawekezaji huvunjwa moyo.
- Miradi ya maendeleo kukwama/kutomalizwa.
- Baadhi ya maeneo ya nchi kupuuzwa kimaendelepo.
- Nchi kukosa misaada.
- Taifa hutumia pesa nyingi kurekebisha ufisadi.
- Sifa za nchi kuharibika.
- uhalifu kuenea/kukosa usalama.
Swali La Tatu
a) Methali: “Matikiti Na Matango Ndiyo Maponya Njaa”
- Hii ni methali.
- Mtahiniwa atunge kisa/visa kuonyesha ukweli wa methali hii.
- Kisa kionyeshe sehemu mbili za methali.
- Upuuzaji/kudunisha kitu, jambo au mtu.
- Kitu, mtu au jambo hilo lije liwe ni la manufaa baadaye wakati wa shida.
b) Msamiati wa methali
- Matikiti na matango = aina ya vyakula visivyothaminiwa sana.
- Maponya = yanayookoa/yanayofaa
- Njaa = shida
c) Maana ya methali
Vitu tunavyodunisha/tunavyopuuza huweza kuwa na msaada mkubwa wakati wa shida. Kitu tulichonacho mkononi mwetu ndicho kinaweza kututoa taabani wakati wa shida, hivyo basi tusikidharau.
Swali La Nne
a) Insha Ya Mdokezo
- Hii ni Insha ya mdokezo na mdokezo huu ni wa kumalizia.
- Mtahiniwa atunge kisa kinachomalizikia kwa dondoo hili.
- Mtahiniwa ajihusishe katika kisa hiki.
- Mtahiniwa atumie nafsi ya kwanza
- Kisa kiwe na tendo/jambo baya kisiri
- Jambo hili linawekwa wazi
- Mhusika anakosa uso yaani anaaibika sana.
b) Methali: “Muungwana akivuliwa nguo huchutama”.
Maana: Uovu wa mtu anayedhaminiwa ni mwema unapofishuliwa yeye huaibika.

helpful