Category Archives: Sarufi

Numbers 1-100 in Kiswahili

  1. Moja
  2. Mbili
  3. Tatu
  4. Nne
  5. Tano
  6. Sita
  7. Saba
  8. Nane
  9. Tisa
  10. Kumi
  11. Kumi na moja
  12. Kumi na mbili
  13. Kumi na tatu
  14. Kumi na nne
  15. Kumi na tano
  16. Kumi na sita
  17. Kumi na saba
  18. Kumi na nane
  19. Kumi na tisa
  20. Ishirini
  21. Ishirini na moja
  22. Ishirini na mbili
  23. Ishirini na tatu
  24. Ishirini na nne
  25. Ishirini na tano
  26. Ishirini na sita
  27. Ishirini na saba
  28. Ishirini na nane
  29. Ishirini na tisa
  30. Thelathini
  31. Thelathini na moja
  32. Thelathini na mbili
  33. Thelathini na tatu
  34. Thelathini na nne
  35. Thelathini na tano
  36. Thelathini na sita
  37. Thelathini na saba
  38. Thelathini na nane
  39. Thelathini na tisa
  40. Arobaini
  41. Arobaini na moja
  42. Arobaini na mbili
  43. Arobaini na tatu
  44. Arobaini na nne
  45. Arobaini na tano
  46. Arobaini na sita
  47. Arobaini na saba
  48. Arobaini na nane
  49. Arobaini na tisa
  50. Hamsini
  51. Hamsini na moja
  52. Hamsini na mbili
  53. Hamsini na tatu
  54. Hamsini na nne
  55. Hamsini na tano
  56. Hamsini na sita
  57. Hamsini na saba
  58. Hamsini na nane
  59. Hamsini na tisa
  60. Sitini
  61. Sitini na moja
  62. Sitini na mbili
  63. Sitini na tatu
  64. Sitini na nne
  65. Sitini na tano
  66. Sitini na sita
  67. Sitini na saba
  68. Sitini na nane
  69. Sitini na tisa
  70. Sabini
  71. Sabini na moja
  72. Sabini na mbili
  73. Sabini na tatu
  74. Sabini na nne
  75. Sabini na tano
  76. Sabini na sita
  77. Sabini na saba
  78. Sabini na nane
  79. Sabini na tisa
  80. Themanini
  81. Themanini na moja
  82. Themanini na mbili
  83. Themanini na tatu
  84. Themanini na nne
  85. Themanini na tano
  86. Themanini na sita
  87. Themanini na saba
  88. Themanini na nane
  89. Themanini na tisa
  90. Tisini
  91. Tisini na moja
  92. Tisini na
  93. Tisini na tatu
  94. Tisini na nne
  95. Tisini na tano
  96. Tisini na sita
  97. Tisini na saba
  98. Tisini na nane
  99. Tisini na tisa
  100. Mia moja

Share this;

Dhana ya Kiima

Kiima huonyesha nomino au kiwakilishi ambacho hufanikisha kutendeka kwa kitendo.

Kwa mfano: Paka anakunywa maziwa.

Nani anakunywa maziwa? Paka. Kwa hivyo paka ndiye mtendaji

Miundo ya kiima

Nomino pekee

Linet anapaka gari rangi.

Kuku anachakura mchangani.

Mwikali anasoma habari.

Nomino+kiunganishi+nomino

Paka na mbwa wemefungiwa pamoja.

Kiongozi na wananchi wanapanda miche.

Nomino +kivumishi

Mtu huyo ana ujuzi mkubwa.

Askari huyo hutii sheria.

Kiwakilishi

Hao husoma vitabu mtandaoni.

Yule atakupigia kesho.

Kiwakilishi + kivumishi

Huyo mkubwa umeleta mvua.

Hayo mengi hayafai.

Nomino na kishazi tegemezi

Mhandisi aliyefanya kazi vizuri amepewa zabuni nyingine.

KUMBUKA

Kiima huweza kutokea katika sehemu yoyote ya sentensi. Aghalabu kihusishi na hutumiwa kuonyesha mtendaji/kiima. Swali hili hutahiniwa sana. Hapa, kiambishi “na <by>” hakitumiki kama kiunganishi.

Mfano: Gari lilioshwa na mgeni wao (kiima)

Katika sentensi hii “Gari” ni shamirisho kipozi ilhali “mgeni wao” ni kiima. Unaweza kuandika : Mgeni wao aliosha gari. Maana haibadiliki. Mtindo huu wa kuandika sentensi kwa Kiingereza huitwa ” Passive and Active voice”

KUMBUKA

Kiima hutokea katika viambishi awali (vitenzi). Huwa ni mofimu inyoonyesha nafsi au mtendaji.

a-na-chor-a, wa-me-kat-a,
Share this;

Matumizi ya kiambishi “na”

Kiambihi kina matumizi yafuatayo katika lugha ya Kiswahili.

Kuonyesha wakati uliopo/wa sasa

Mfano: Rais anahutubia wananchi.

Omondo anapiga simu.

Kiunganishi (Kuunganisha maneno, virai, vishazi,sentensi)

Mfano: Joseph na Maria wamechguliwa.

Wao hufuga wanyama na kupanda mimema.

Kuonyesha kihusishi cha mtenda

Mfano: Atapelekwa kanisani na Mjomba

Wageni watakaribishwa na waziri wa afya.

Kitenzi kishirikishi kipungufu

Mfano: Mtu huyo ana sifa nyingi.

Watoto wana ujuzi wa hali ya juu.

Mnakaribishwa kuongezea matumizi mengine.

Share this;