Category Archives: Kiswahili

Viambishi

Maana ya kiambishi

  • Ni mofimuinayoongezwa kabla au baada ya mzizi wa neno ili kuleta maana iliyokusudiwa.
  • Kiambishi ni kipande cha neno chenye maana ya kisarufi ambacho huongezwa kabla au baada ya mzizi wa neno ili kuleta maana iliyokusudiwa.

    Kuna aina mbili za viambishi

    1. Kiambishi awali
    2. Kiambishi tamati

    Kumbuka kuwa:

    Mzizi ni sehemu ya neno ambayo huongezwa viambishi.

    Mfano:

    • Wa-tu / m-toto :(nomino)
    • A-na-chez-a/ a-ta-pik-a :(kitenzi)

    Viambishi awali hutumika kuonyesha:

    1. Ngeli
    2. Kiima/mtenda
    3. Nafsi
    4. Wakati
    5. Yambwa(mtendwa/ mtendewa)
    6. Hali (timilifu/mazoea/isiyod hihirika/masharti)
    7. Kirejeshi
    8. Kikanushi
    9. Umoja/wingi
    10. Ukubwa/udogo wa nomino

    Mifano ya Vikanushi

    Viambishi tamati hutumika kuonyesha:

    1. kirejeshi
    2. kiulizi
    3. Kauli/mnyambuliko
    4. Kiishio
    5. Uundaji wa nomino

    Kubainisha viambishi

    Mfano 1

    Mfano 2

    Mfano 3

    Mfano 4

    Mfano 5

    a)Onyesha viambishi awali na viambishi tamati

    b) Bainisha majukumu ya viambishi ulivyotambua

    • ViatuWalipochezaTegewaHakumpigaAnyweshavyoAlimdharau

    • jigari

    Majibu

    1. Viatu: awali; vi
    2. Walipocheza- awali:wa,li,po tamati: a
    3. Tegewa: –                                      tamati: ew, a
    4. Hakumpiga- awali:ha,ku,m                                      tamati: a
    5. Anyweshavyo- awali: a                              tamati:esh, a, vyo
    6. alimdharau- awali:a,li,m
    7. jigari: awali; ji


    Share this;

    Namna ya kulezea mandhari

    Mandhari Katika Fasihi

    MAANA

    Ni sehemu ambapo au mazingira ambako matukio ya hadithi au masimulizi yanafaanyika.

    Kazi ya fasihi hujengwa katika mazingira maalum ambayo huitwa mandhari.

    UFAFANUZI

    • Mandhari katika kazi ya fashi husaidia kuleta hisia iliyokusudiwa.
    • Mfano kama msanii anakusudia kuleta hisia ya woga humlazimu kuchukua mandhari ya woga kama msitu mnene, ngurumo za wanyama wakali.
    • Huonyesha jamii,mahali,wakati wa kihistoria na hali ya maisha ambambo mwandishi anaandika kazi yake.
    • Mandhari ya riwaya ni mapana na yanayoendelezwa kikamilifu kwa sababu riwaya hujihusisha na vipengele vingi vya maisha ambavyo hupatikana katika nyakati na mahali tofauti kama vile

    shuleni,mijini,vijijini,ng’ambo….

    • Hali mbalimbali pia huweza kujitokeza.kwa mfano, hali ya huzuni, furaha,ufanisi,kupungukiwa,kufiwa…..
    • Mandhari husaidia kueleza maudhui na dhamira ya mwandishi.
    • Maudhui ya kazi lazima yelenge kipindi cha wakati ambapo kazi imeandikwa

    Vipengele vya mandhari

    1. Wakati wa kutukia kwa matendo
    2. Kutambulisha wahusika.
    3. Kuonyesha migogoro.
    4. Kuonyesha matatizo ya kijamii- ulevi,ufisadi,wizi.
    5. Kueleza mahali pa tukio.
    6. Kuonyesha taharuki.
    • Kuonyesha maudhui
    • Kuonyesha hali- hali ya huzuni.
    • Kuonyesha kipindi cha wakati-wakati wa ukoloni
    • Kuonyesha utamaduni wa jamii
    • Kulinganua hali za matabaka.
    • Kuonyesha hali ya kiuchumi- je kuna mgao sawa wa mali

    SWALI

    “ Najihisi kama Kurwa katika novella ya Kurwa na Doto”

    Eleza umuhimu wa nafsineni katika kufanikisha mandhari katika riwaya ya Chozi la Heri.

    JIBU

    1. Mandhari huashiria mahali – kupitia mhusika umu tunaona anasomea shule ya tangamano pamoja na wanafunzi wenzake.
    2. Mandhari huashiria wakati – kupitia umu tunapata wasichana wanne bwenini wakielezana matatizo
    3. Mandhari huashiria wahusika – kupitia umu tunaona utepetevu wa askari kazini
    4. Mandhari huchimuza maudhui – kuptia umu tunapata maudhui ya changamoto za malezi anapoachwa na wanuna wake katika mlima wa simba
    5. Mandhari huibua taharuki – umu anatuonyesha kwao kulikuwa mlima wa simba babake alikozikwa hatujui kama waliwahi rudi huko tena
    6. Mandhari huonyesha hali – kupitia umu tunapata hali ya masikitiko wanayopitia wanafunzi pale shule ya Tangamano
    7. Mandhari huashiri tabaka – kupitia mandhari ya nyumbani mwa mwnageka anakopangwa umu kunaashiria tabaka la juu
    Share this;

    Kutambua aina ya shairi

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

    Hapa duniani, moyo unaimba
    Mioyo yetu yakutane, furaha tutaona
    Pamoja, tusimame, tukishirikiana
    Nchi yetu tukuzwe, kwa upendo tuunganishe.

    Mawingu yananing’aa, jua likiangaza
    Safari yetu ya maisha, kila siku ni zawadi
    Kwa upendo na matumaini, tutaendelea mbele
    Kupitia changamoto zote, tutashinda kwa pamoja.

    Nchi yetu, yenye utajiri ,wa asili na tamaduni
    Sijali rangi, lugha, au dini tunazofuata
    Kwa umoja na amani, tuwe kitu kimoja
    Tuwepo kwa wenzetu, kwa kila mtu, tuwapende.

    Kwa Swahili yetu, tulinde na tuhifadhi
    Historia yetu, tunayoipenda na kujivunia
    Tukumbuke waliotangulia, na kuwaongoza vizazi vyetu
    Nchi yetu, taifa letu, kwa daima tutakuwa pamoja.

    Maswali
    a) Pendekeza kichwa cha shairi hili. (alama 1)
    b) Tambua aina ya shairi hili. (alama 2)
    c) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
    d) Fafanua Bahari katika shairi hili kwa kurejelea idadi ya mishororo. (alama 1)
    e) Tambua mbinu zozote mbili ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi. (alama 2)
    f) Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 1)
    g) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)
    h) Tambua mbinu mbili za kimtindo zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
    i) Onyesha aina za urudiaji zinazojitokea katika shairi hili. (alama 2)
    j) Tambua nafsi neni katika shairi hili. (alama 1)

    Majibu

    a)Pendekeza kichwa cha shairi hili. (alama 1)
    Tuipende nchi yetu


    b)Tambua aina ya shairi hili. (alama 2)
    Shiri huru- idadi ya vipande katika mishororo hailingani


    c)Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
    -Lina beti nne
    -Kila ubeti una mishororo minne
    -Idadi ya vina ni tofauti katika baadhi ya mishororo
    -Idadi ya vipande ni tofauti katika baadhi ya mishororo.


    d)Fafanua Bahari katika shairi hili kwa kurejelea idadi ya mishororo. (alama 1)
    – Tarbia- kila ubeti una mishororo minne


    c)Tambua mbinu zozote mbili ambazo mshairi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi. (alama 2)
    -Kuboronga sarufi- “hapa duniani moyo unaimba” badala ya “moyo unaimba hapa duniani”
    -Inkisari- sijali badala ya usijali/tusijali


    d)Eleza dhamira ya shairi hili. (alama 1)
    Anawahamasisha wananchi kuishi kwa umoja, kuwa na matumaini, upendo na kuhifadhi historia yao.


    e)Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)
    Nchi yetu ina utajiri wa asili na tamaduni. Tusijali rangi, lugha, au dini tunazofuata. Kwa umoja na amani tuwe kitu kimoja. Tuwepo kwa wenzetu na tuwapende.


    f)Tambua mbinu mbili za kimtindo zilizotumika katika shairi hili. (alama 2)
    -Uhaishaji- moyo unaimba
    -Stiari- safari yetu ya maisha ni zawadi


    g)Onyesha aina za urudiaji zinazojitokea katika shairi hili. (alama 2)
    -Urudiaji wa neno- yetu
    -Urudiaji wa kifungu cha maneno- nchi yetu


    h)Tambua nafsi neni katika shairi hili. (alama 1)
    Mzalendo/mtu anayeipenda nchi yake- Nchi yetu, taifa letu, kwa daima tutakuwa pamoja.

    Share this;