Category Archives: Lessons

Nafasi ya Lugha ya Kiswahili Duniani

Kiswahili ni lugha inayozungumzwa na watu zaidi ya milioni 150 duniani kote. Lugha hii ina majukumu mbalimbali ambayo inatekeleza:

  1. Lugha ya kikanda: Kiswahili ni lugha rasmi ya Ummoja wa Afrika(AU) na Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)
  2. Pia, Kiswahili ni lugha inayotumiwa sana katika nchi za Afrika Mashariki na Kati kama vile Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, na Congo.
  3. Lugha ya mawasiliano: Kiswahili ni lugha ya mawasiliano ya kawaida katika Afrika Mashariki na Kati. Inatumika katika shughuli za biashara, utalii, utamaduni na kijamii.
  4. Lugha ya elimu: Kiswahili ni lugha rasmi ya elimu nchini Tanzania na Kenya. Pia, Kiswahili ni somo la lazima katika shule nyingi Afrika Mashariki. Kiswahili pia Kinafunzwa katika vyuo mbalimbali nchini.
  5. Lugha ya utamaduni: Kiswahili ni lugha ya utamaduni na sanaa. Inatumika katika fasihi, muziki, filamu na maonyesho mengine ya sanaa. Pia, Kiswahili ni lugha inayotumiwa katika maandishi ya kidini na kifalsafa.
  6. Utangazaji: Kiswahili kinatumika katika vyombo vya habari duniania kama vile; Redio China Kimataifa na VOA Swahili.

Katika kuyafanya majukumu yote hayo, Kiswahili kinazidi kupata umaarufu duniani kote.

Share this;

Umuhimu wa amani katika jamii

Amani ni moja ya mambo muhimu zaidi katika maisha ya mwanadamu. Inamaanisha kuwa na utulivu wa akili, kutokuwa na wasiwasi, na kuishi bila hofu ya ghasia na vurugu. Amani inaathiri kila nyanja ya maisha yetu, iwe ni katika mahusiano yetu ya kibinafsi, kazi, au katika jamii.

Kwanza kabisa, amani inawezesha watu kuishi kwa usalama. Watu wanapohisi kwa usalama, wanaweza kufikia uwezo wao kamili. Wanaweza kufanya kazi zao kwa uhuru, kufikiria kwa uhuru na kuendeleza talanta zetu kikamilifu. Watu hawatakiwi kuishi wakiwa na hofu ya kufukuzwa au kushambuliwa, ambayo inaweza kuzuia maendeleo yao na kuleta athari mbaya kwa afya yao ya kiakili.

Pili, amani ni muhimu sana kwa maendeleo ya uchumi. Nchi zenye amani mara nyingi huwa na uchumi imara. Uchumi unaweza kukua kwa kasi zaidi katika mazingira yenye amani, ambayo inaleta fursa zaidi za ajira na kupunguza umaskini. Kwa hivyo, amani inachangia kuboresha maisha ya watu kwa njia nyingi.

Tatu, amani inawezesha ushirikiano wa kitaifa na kudumisha uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa mbalimbali. Nchi zenye amani zinaweza kushirikiana kwa karibu katika biashara, utamaduni na maendeleo. Hii inasaidia kujenga uhusiano mzuri kati ya nchi na kupunguza uwezekano wa migogoro ya kimataifa.

Hatimaye, amani inasaidia kudumisha mazingira mazuri ya kulea watoto wetu. Watoto wanaoheshimiwa na kuishi katika mazingira ya amani wana uwezekano mkubwa wa kuwa watu wazima wanaojitambua na wenye heshima kwa wengine.

Kwa kuhitimisha, amani ni muhimu kwa kila mtu na kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Tunapaswa kufanya kazi kwa pamoja kudumisha amani katika maisha yetu ya kila siku na katika jamii yetu ili kujenga ulimwengu bora kwa vizazi vijavyo.

Share this;

Dhana ya Kiima

Kiima huonyesha nomino au kiwakilishi ambacho hufanikisha kutendeka kwa kitendo.

Kwa mfano: Paka anakunywa maziwa.

Nani anakunywa maziwa? Paka. Kwa hivyo paka ndiye mtendaji

Miundo ya kiima

Nomino pekee

Linet anapaka gari rangi.

Kuku anachakura mchangani.

Mwikali anasoma habari.

Nomino+kiunganishi+nomino

Paka na mbwa wemefungiwa pamoja.

Kiongozi na wananchi wanapanda miche.

Nomino +kivumishi

Mtu huyo ana ujuzi mkubwa.

Askari huyo hutii sheria.

Kiwakilishi

Hao husoma vitabu mtandaoni.

Yule atakupigia kesho.

Kiwakilishi + kivumishi

Huyo mkubwa umeleta mvua.

Hayo mengi hayafai.

Nomino na kishazi tegemezi

Mhandisi aliyefanya kazi vizuri amepewa zabuni nyingine.

KUMBUKA

Kiima huweza kutokea katika sehemu yoyote ya sentensi. Aghalabu kihusishi na hutumiwa kuonyesha mtendaji/kiima. Swali hili hutahiniwa sana. Hapa, kiambishi “na <by>” hakitumiki kama kiunganishi.

Mfano: Gari lilioshwa na mgeni wao (kiima)

Katika sentensi hii “Gari” ni shamirisho kipozi ilhali “mgeni wao” ni kiima. Unaweza kuandika : Mgeni wao aliosha gari. Maana haibadiliki. Mtindo huu wa kuandika sentensi kwa Kiingereza huitwa ” Passive and Active voice”

KUMBUKA

Kiima hutokea katika viambishi awali (vitenzi). Huwa ni mofimu inyoonyesha nafsi au mtendaji.

a-na-chor-a, wa-me-kat-a,
Share this;