Silabi ni kipashio kinachotamkika
Maana
Sauti mbili au zaidi zinazotamkwa kwa pamoja.
Sauti mbili au zaidi ambazo hutamkwa kama fungu moja la sauti.
Aina za silabi
Kuna aina mbili za sila katika Kiswahili
Silabi funge
Hizi ni silabi ambazo huishwa kwa konsonanti
Mfano: m-tu
Silabi wazi/huru
Hizi ni silabi ambazo huishia kwa irabu
Mfano: ka-ka, le-o,u-si-ku
MUUNDO WA SILABI
Kuna miundo mbalimbali ya silabi katika Kiswahil
Irabu pekee
o-a,i-ta
konsonanti pekee
m-tu
konsonanti irabu
ji-tu
konsonanti konsonanti irabu
fye-ka, bwe-ka
konsonanti konsonanti konsonanti irabu
mbwe-ha,twa-ngwa
Mifano ya maswali
- Eleza maana ya silabi.(alama 1)
- Huku ukitoa mifano eleza aina mbili za silabi. (alama 2)
- Eleza miundo yoyote miwili ya silabi. (alama 2)
- Tenganisha silabi: viyeyusho (alama 2)
- Tunga neno lenye muundo ufuatao: KI+KI+I. (alama 2)

Mfano wa silabi funge si sahihi! Silabi funge humalizikia kwa konsonanti sio kuwa pekee! K.m. dak-ta-ri, il-ha-li, muf-ti ndiyo mifano sahihi.
Asante kwa maoni yako.
Karibu
Pia lab-da ni mfano sahihi
Asante
Karibu!
Neno Oktoba na pia neno mmea litasilabishwa aje tafadhali?
Ok-to-ba
M-me-a
Xwa sana
swadakta
Nimefaidika
Silabi za konsonanti , konsonanti,nusu irabu na irabu
Maneno ambayo yanashirikisha silabi zenye muundo huu ni machache sana katika lugha ya kiswahili.
mfano ni;
Mbwe-ha
Alipi-ngwa
Cha-ngwa
Mbwi-to-mbwi-to.
Mwisho ni , kuna silabi funge
Silabi funge hujitokeza sana sana katika maneno ya kukopwa
mfano ni
daf-tari
lab-da
Alhamisi
inkshafi
Nkt.
There is a wonderfull or quite
teaching from this site,thanks.
Nami naomba msaada wenu hapa. Maneno yafuatayo ya silabi ngapi: JAMVI na KABLA
Jam-vi na kab-la